Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Timotheo 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 LAKINI ujue neno hili, ya kuwa siku za mwisho zitakuwa nyakati za khatari.

2 Maana watu walakuwa wenye kujipenda nafsi zao, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kufuru, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao,

3 wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,

4 makhaini, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko Mungu;

5 wenye mfano wa utawa, lakini wakikana nguvu zake; ujiepushe na hao.

6 Kwa maana katika hawa wamo wale wajiingizao kalika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi,

7 wakijifunza siku zote, wasiweze kabisa kufikia ujuzi wa kweli.

8 Vile vile kama Yanne na Yambre walivyopingana na Mnsa, vivyo hivyo na hawa wapingana na kweli, ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.

9 Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote kama na wa hao ulivyokuwa.

10 Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na upole, na upendo, na uvumilivu,

11 tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote.

12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya ntawa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

13 Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na wakidanganyika.

14 Bali wewe ukae katika yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni nani ambae ulijifunza kwake,

15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.

16 Killa andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibu katika haki;

17 illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo