2 Timotheo 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 BASSI wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu. 2 Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine. 3 Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Yesu Kristo. 4 Hakuna mfanya vita ajitiae katika shughuli za dunia; illi ampendeze yeye aliyemwandika awe askari. 5 Hatta mtu akishindana hapewi taji asiposhindana kwa halali. 6 Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kuyashiriki matunda. 7 Yafahamu sana hayo nisemayo, maana Bwana atakupa akili katika mambo yote. 8 Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daud, kama inenavyo injili yangu. 9 Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi. 10 Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele. 11 Neno hili ni neno la kuaminiwa. Maana kama tukifa pamoja nae, tutaishi pamoja nae pia; 12 kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi: 13 ikiwa hatuamini, yeye hudumu kuwa mwaminifu, hawezi kujikana nafsi yake. 14 Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao. 15 Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu. 16 Jiepushe na maneno yasiyo na maana, yasiyo ya dini; maana wataendelea zaidi katika maovu; 17 na neno lao litakuwa likitafuna kama donda ndugu. Katika hao ni Humenayo na Fileto, 18 walioikosa kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, nao waipindua imani ya watu wengine. 19 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu. 20 Bassi katika nyumba havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina heshima. 21 Bassi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hawa atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa killa kazi iliyo njema. 22 Lakini zikimbie tamaa za ujana; nkafuate haki, na imani, na uaminifu, na upendo, na amani, pamoja na hao wamwitiao Bwana kwa moyo safi. 23 Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi: 24 Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezae kufundisha, mvumilivu, 25 akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli, 26 wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Shetani, wamepatikana wahayi nae, hatta kuyafanya apendayo Mungu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania