2 Timotheo 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kama alivyopenda Mungu, kwa ahadi ya uzima ulio katika Yesu Kristo: 2 kwa Timotheo mwanangu mpendwa; Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. 3 Namshukuru Mungu, nimwabuduye tangu zamani za wazee wangu kwa dhamiri safi, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu, mchana na usiku, ninatamani sana kukuona, 4 nikikumbuka machozi yako, illi nijae furaha; 5 nikikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, iliyokaa kwanza katika bibi yako Loi, na katika mama yako Euniki; aa ninasadiki ya kwamba na wewe nawe unayo. 6 Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. 7 Maana Mungu hakutupa roho ya khofu, bali ya nguvu na ya upendo ua ya moyo wa kiasi. 8 Bassi usiutahayarikie ushuhuda wa Bwana wetu, wala mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja na Injili kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; 9 aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani; 10 na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyebatili mauti na kuufunua uzima ua kutoa kuharibika, kwa ile Injili, 11 aliyonifauya mkhubiri na mtume na mwalimu wa mataifa. 12 Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile. 13 Shika sura ya maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo uiio katika Kristo Yesu. 14 Ilinde ile amana nzuri kwa Rolio Mtakatifu akaae ndani yetu. 15 Wajua hili, ya kuwa wote walio katika Asia wameniacha, katika hao ni Figello na Hermogene. 16 Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu; 17 bali, alipokuwa katika Rumi, alinitafuta kwa bidii, akanipata. 18 Bwana na ampe kuona rehema kwa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonikhudumia katika Efeso, wewe wajua sana. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania