Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Petro 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAPENZI, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika hizo naziamsha nia zenu sali kwa kuwakumbusheni,

2 mpate kuyakumbuka maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana Mwokozi iliyoletwa na mitume wake.

3 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,

4 na kusema, iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali hiyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.

5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili, ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na inchi pia, imefanyizwa kwa maji ikatoka katika maji, kwa neno la Mungu;

6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na inchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hatta siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wana Adamn wasiomcha Mungu.

8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu kama siku moja.

9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wahesabuvyo kukawia, bali huvumilia kwenu, hapendi mtu aliye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

10 Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Bassi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na ntawa,

12 mkitazamia hatta ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka.

13 Lakini, kwa sababu ya ahadi yake tunatazamia mbingu mpya na inchi mpya, ambayo haki itakaa ndani yake.

14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.

15 Na ubasibuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa wokofu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paolo alivyowaandlkieni kwa hekima aliyopewa;

16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa khabari za mambo hayo mumo humo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa upotevu wao wenyewe.

17 Bassi, wapenzi, mkitangulla kujua haya, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hawo wakhalifu, mkaanguka na kuuacha uthubutifu wenu.

18 Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo