2 Petro 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 LAKINI kuliondoka manabii wa uwongo katika watu, kama vile kwenu kutakavyokuwa waalimu wa uwongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hatta Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu nsiokawia. 2 Na wengi watafuata jeuri zao; kwa hawo njia ya kweli itanenwa unajisi. 3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii. 4 Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu; 5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa wasiomeha Mungu, 6 akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipiudua ua kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya; 7 akamwokoa Lut, aliyehuzunishwa na mwenendo wa uasharati wa hawo wakhalifu; 8 maaua mtu huyu mwenye haki akikaa kwao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sharia: 9 Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu; 10 na khassa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka. Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; 11 ijapokuwa malaika, walio wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele ya Bwana. 12 Lakini hawo kama nyama wasio na akili, kwa asili yao watu wa kukamatwa kama nyama na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao; 13 wakipatwa na madhara, ujira wa udhalimu wao, wakidhani kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; ni mawaa na aibu, wakifuata anasa katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi; 14 wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kukhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo ilivozoezwa kutamani, wana wa laana; 15 walioiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaam, mwana wa Bosor, aliyependa ujira wa ndhalimu: 16 lakini alikaripiwa kwa ukhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule. 17 Hawa ni visiwa visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa: 18 wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu: 19 wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu. Maana mtu akishindwa na mtu, huwa mtumwa wa mtu yule. 20 Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua sana Bwana, Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. 21 Maana ingekuwa kheri kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua ile amri takatifu waliyopewa na kuiacha. 22 Lakini lile onyo la ile methali ya kweli limewapata: Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa kujifingirisha matopeni. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania