Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Petro 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

2 Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu;

3 kwa kuwa uweza wa Mungu umetukarimia vitu vyote vyenye uzima na utawa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe;

4 kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

5 Naam, na kwa sababu hiyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenn tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,

6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu uvumilivu, na katika uvumilivu wenu utawa,

7 na katika utawa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.

8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.

9 Maana yeye asiyekuwa na haya ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.

10 Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.

11 Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuuingia ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.

12 Kwa hiyo sitakosa kuwakumbusheni hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthubutishwa katika kweli iliyowatikia.

13 Nami naona ni haki, maadam nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsheni kwa kuwakumhusheni.

14 Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha kwa wazi.

15 Walakini nitajitahidi, illi killa wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo haya.

16 Maana hatukufuata hadithi zilozotungwa kwa werevu, tulipowajulislia ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa mashahidi wa ukuu wake.

17 Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, ya kama, Huyu ndiye mwanangu nimpendae, amhae nimependezwa nae.

18 Na santi hii ndiyo tuliyoisikia tulipokuwa pamoja uae katika mlima ule mtakatifu.

19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ingʼaayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya assubuhi kuzuka mioyoni mwenu.

20 Mkijua neno hili ya kwamba hapana unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fullani tu.

21 Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo