1 Yohana 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae. 2 Hivi twajua kwamba twawapencla watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. 3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kuzisinka amri zake: na amri zake si nzito. 4 Kwa maana killa kitu kilihozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, imani yetu. 5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa yeye aaminiye ya kwamba Yesu yu Mwana wa Mungu? 6 Huyu ndiye ajae kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Na Roho ndiyo ishuhuduyo, kwa sababu Roho ndiyo iliyo kweli. 7 Kwa maana watatu ni mashahidi mbinguni, Baba, Neno, na Robo Mtakatifu, ua watatu hawa ni umoja. 8 Maana watatu ndio washuhuduo duniani, roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupataua kwa khabari moja. 9 Tukiupokea ushuliuda wa wana Adamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, amemshuhudia Mwana wake. 10 Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu amemsbuhudia Mwana wake. 11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwana wake. 12 Aliye nae Mwana, ana uzima; asiye nae Mwana wa Mungu hana uzima. 13 Nimewaandikia mambo haya, illi mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. 14 Na huu ndio njasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu kama vile apendavyo, atusikia: 15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombapo cho chote, twajua kwamba tunazo zile dua tulizomwomba. 16 Mtu akimwona ndugu yake anakosa kosa lisilo la mauti, ataomba, nae atampa uzima kwa ajili ya hawo wakosao kosa lisilo la mauti. Liko kosa lililo la mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hilo. 17 Killa lisilo la haki ni kosa, na kosa liko lisilo la mauti. 18 Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi. 19 Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. 20 Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele. 21 Watoto wangu wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania