Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Yohana 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WATOTO wangu wadogo, nawaandikia haya illi msitende dhambi. Na ijapo mtu akatenda dhambi tuna Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,

2 nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.

3 Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake.

4 Yeye asemae, Nimemjua, nae hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.

5 Lakiui yeye alishikae neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Ilivi twajua ya kuwa tumo ndani yake.

6 Yeye asemae ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vilevile kama yeye alivyoenenda.

7 Ndugu, siwaandikii amri mpya, illa amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo.

8 Na ile amri ya zamani ndiyo ile mliyosikia tangu mwanzo. Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kungʼaa.

9 Yeye asemae kwamba yumo katika nuru, nae amchukia ndugu yake, yumo gizani hatta sasa.

10 Yeye ampendae ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.

11 Bali yeye amchukiae ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.

12 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.

13 Nawaandikia, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nawaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba.

14 Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu m hodari, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.

15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16 Maana killa kilichomo duniani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, hazitokani na Baba, bali zatokana ua dunia.

17 Na dunia inapita, na tamaa yake, bali yeye afanyae mapenzi ya Mungu adumu hatta milele.

18 Watoto, ni wakati wa mwisho: na kama vile mlivyosikia kwamba adui wa Kristo yuaja, hatta sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.

19 Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

20 Na ninyi mmepakwa mafuta nae aliye Mtakatifu na mnajua yote.

21 Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamwijui kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uwongo wo wote utokao katika kweli.

22 Naui aliye mwongo illa yeye akanae ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye adui wa Kristo, amkanae Baba na Mwana.

23 Killa anikanae Mwana, amkana Baba pia.

24 Bassi, na yakae ndani yenu maneno yale mliyoyasikia tangu mwanzo. Neno lile mlilolisikia tangu mwanzo likikaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.

25 Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele.

26 Nimewaandikia haya katika khabari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.

27 Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake.

28 Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, illi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibishwe mbele zake katika kuja kwake.

29 Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo