1 Yohana 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 ILIYOKUWA tangu mwanzo, tuliyoisikia, tuliyoiona kwa macho yetu, tuliyoitazama, na mikono yetu ikaipapasa, kwa khabari ya Neno la uzima, 2 (na uzima buo ulidhihirika, nasi tumeona, na twashuhudu, na twawakhubirini ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 4 Na haya twawaandikieni, illi furaha yenu itimizwe. 5 Na hii ndiyo khabari tuliyoisikia kwake, na kuikhubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza yo yote hamna ndani yake. 6 Tukisema twashirikiana nae, tena tukienenda gizani, twasema uwongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; 7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote. 8 Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya, wala kweli haimo mwetu. 9 Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote. 10 Tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya mwongo wala neno lake halimo mwetu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania