1 Wathesalonike 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 LAKINI kwa khabari ya nyakati na majira, ndugu, hamna haja niwaandikie. 2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku. 3 Maana wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo niwenye mimba; nao hawataokolewa. 4 Bali ninyi, ndugu, hamwi katika giza, siku ile iwapale kama mwizi. 5 Maana ninyi nyote wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi hatuwi wa usiku, wala wa giza. 6 Bassi tusilale kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. 7 Maana walalao hulala usiku, na walewao hulewa usiku. 8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, tukijivika kifuani imani na upendo, na chepeo yetu iwe tumaini la wokofu. 9 Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, 10 aliyekufa kwa ajili vetu, illi tuishi pamoja nae, ikiwa twakesha au ikiwa twalala. 11 Bassi, farijianeni mkajengeane, killa mtu mwenzake, vile vile kama mnavyofanya. 12 Lakini, ndugu, tunataka mwajue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu na kuwasimamieni katika Bwana, na kuwaonyeni; 13 mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Mwe na amani ninyi kwa ninyi. 14 Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote. 15 Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. 16 Furahini siku zote; 17 ombeni hila kukonia; 18 shukuruni kwa killa jambo; maana haya ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 19 Msimzimishe Roho; 20 msitweze unabii; 21 jaribuni vyote; lishikeni lililo jema; 22 jitengeni na ubaya wa killa namna. 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye ni mwaminifu awaitae, nae atafanya. 25 Ndugu, tuombeeni. 26 Wasalimuni ndugu kwa husu takatifu. 27 Nawaapisha kwa Bwana, wasomewe ndugu wote waraka huu. 28 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi. Amin. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania