Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wathesalonike 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 MAANA ninyi wenyewe, udugu, mwakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa burre,

2 bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.

3 Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu wala ya uchafu, wala ya hila,

4 bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuaminiwe Injili ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wana Adamu bali Mungu anaetupima mioyo yetu.

5 Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya kuficha tamaa; Muugu ni shahidi.

6 Hatukutaka kusifiwa na watia Adamu, wala na ninyi, wala na wengine, tulipokuwa tuliweza kuwalemea kama mitume wa Kristo;

7 bali tulikuwa wapole kati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.

8 Vivyo hivyo sisi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapeni, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.

9 Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu, tukawakhubirini bivi Injili ya Mungu.

10 Ninyi mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;

11 vile vile kama mjuavyo jinsi tulivyomwonya killa mmoja wemi kama baba amwonavyo mtoto wake, tukiwatieni moyo na kushuhudia,

12 illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.

13 Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.

14 Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi;

15 waliomwua Bwana Yesu na manabii wao wenyewe na kutuudhi sisi, wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;

16 wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho.

17 Lakini sisi, ndugu, tukifarakana nanyi kwa kitambo, kwa nso si kwa moyo, tulitamani zaidi kuwaona nyuso zenu, kwa shauku nyingi.

18 Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paolo, marra ya kwanza, na marra ya pili. Shelani akatuzuia.

19 Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake?

20 Maana ninyi utukufu wetu, na furaha yetu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo