Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 JE! mimi si mtume? mimi si huru? sikumwona Yesu Kristo Bwana wetu? ninyi si kazi yangu katika Bwana?

2 Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, illakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana muhuri ya utume wangu ni ninyi katika Bwana.

3 Jawabu yangu kwa wale wanaoniuliza ni hii.

4 Je! hatuna uwezo wa kula na kunywa?

5 Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?

6 Au je! ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo kutokufanya kazi?

7 Nani aendae vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Nani apandae mizabibu asiokula baadhi ya matunda yake? Au nani achungae kundi, asiyekula haadhi ya maziwa ya kundi?

8 Je! ninanena haya kama mwana Adamu? Au sharia nayo haisemi yayo hayo?

9 Kwa maana katika sharia ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ngʼombe apurae nafaka. Je! Mungu aangalia mambo ya ngʼombe?

10 Au anena hayo kwa ajili yetu bassi? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu kama alimae nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini; nae apurae nafaka kwa matumaini ni haki yake kupata sehemu ya matumaini yake.

11 Ikiwa sisi twaliwapandieni vitu vya rohoni, je! ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?

12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huu; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Injili ya Kristo.

13 Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula sehemu ya vitu vya hekalu, na wale waikhudumiao madhbahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhbahu?

14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waikhubirio Injili wamzukiwe kwa Injili.

15 Lakini sikutumia mambo haya hatta moja. Wala sikuvaandika haya illi iwe hivyo kwangu; maana ni kheri nife kuliko mtu aliye vote abatilishe huku kujisihi kwangu.

16 Maana, ijapokuwa naikhubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimepewa sharti; tena ole wangu nisipoikhubiri.

17 Maana nikiitenda kazi hii kwa khiari yangu nina thawabu; kama si kwa khiari yangu, illakini nimeaminiwa uwakili.

18 Bassi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nikhubiripo, nitatoa Injili ya Kristo bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu haki yangu niliyo nayo katika Injili.

19 Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, illi nipate watu wengi zaidi.

20 Nalikuwa Myahudi kwa Wayahudi, illi niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sharia, nalikuwa kama chini ya sharia, illi niwapate walio chini ya sharia.

21 Kwa wale wasio na sharia nalikuwa kama sina sharia. Si kana kwamba sina sharia mbele za Mungu, hali mwenye sharia mbele za Kristo, illi niwapate wasio na sharia.

22 Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, illi niwapate wanyonge. Nalikuwa mtu wa hali zote kwa watu wote, illi nipate kuwaokoa watu kwa njia zote.

23 Nami nafanya haya yote kwa ajili ya Injili nipate kuishiriki pamoja na wengine.

24 Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.

25 Na killa ashindanae hujiweza katika yote: bassi hao kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi isiyoharibika.

26 Hatta mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitae; napigana vivyo hivyo, si kama apigae hewa:

27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwakhubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo