Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NA kwa khabari ya vitu, vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna elimu. Elimu huleta majivuno, bali upendo hujenga.

2 Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.

3 Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejuliwa nae.

4 Bassi, kwa khabari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hapana Mungu mwingine illa mmoja tu.

5 Kwa maana ijapokuwa wako waitwao waungu, ikiwa mbinguni au duniani, kama vile wako waungu wengi na bwana wengi;

6 illakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu, aliye Baba, ambae vitu vyote vimetokana nae, na sisi twarejea kwake; na yuko Bwana mmoja Yesu Kristo, ambae kwa sabiki yake vitu vyote vimekuwa, na sisi kwa sabiki yake.

7 Bali elimu hii haimo ndani ya watu wote; illa wengine kwa kuizoelea ile sanamu hatta sasa hula kama ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri yao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika.

8 Lakini chakula hakituleti mbele ya Mungu; maana, tukila, hatuongezewi kitu, na tusipokula hatupunguziwi kitu.

9 Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaze wale walio dhaifu.

10 Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na elimu, umeketi chakulani ndani ya hekalu ya sanamu, je! dhamiri yake mtu huyu, kwa kuwa yu dhaifu, haitathubutika hatta ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?

11 Na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa elimu yako, nae ni ndugu ambae Kristo alikufa kwa ajili yake.

12 Na hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuwajeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo.

13 Kwa hiyo, chakula kikimkosesha ndugu yangu, sitakula nyama hatta milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo