Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 YAKINI khabari imeenea ya kama kwenu kuna zina, na zina hiyo ya namna isiyonenwa hatta katika mataifa, kwamba mtu awe na mke wa baba yake.

2 Nanyi minejivuna wala hamkusikitika illi aondolewe kati yenu yeye aliyetenda jambo hilo.

3 Kwa maana mimi kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.

4 Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na nweza wa Bwana wetu Yesu Kristo,

5 kumtolea Shetani mtu huyo, mwili uadhibiwe, illi roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.

6 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima?

7 Bassi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, illi mwe donge jipya, kama vule mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka yetu amekwisha kutolewa sadaka kwa ajili yetu, yaani Kristo;

8 bassi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochacha, ndio weupe wa moyo na kweli.

9 Naliwaandikieni katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.

10 Sisemi msichangamane kabisa kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani an wanyangʼanyi, an wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.

11 Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae.

12 Maana yanikhusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu walio ndani?

13 Bali hao walio nje Mungu atawahukumu. Mwondoeni mtu yule mbaya, asikae kwenu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo