Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 MTU na atubesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.

2 Tena inayohitajiwa katika mawakili, ndio mtu aonekane amini.

3 Kwangu, lakini, si kitu kabisa nibukumiwe na ninyi, ama na hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hatta nafsi yangu.

4 Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabikiwi haki kwa ajili hiyo; illa aninukumuye ni Bwana.

5 Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

6 Mambo haya, ndugu, nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na wa Apollo kwa ajili yemi, illi kwa khabari zetu mpate kujifunza katika fikara zenu kutokuruka mpaka wa yale yaliyoandikwa; mtu mmoja asijivune juu ya mwenziwe, kwa ajili ya mtu mwingine.

7 Maana ni nani anaekupambanua na mwingine? na una, nini usiyoipokea? Na iwapo uliipokea, wajisifiani kana kwamba hukuipokea?

8 Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Na ingekuwa kheri kama mngalimiliki, illi sisi nasi tumiliki pamoja nanyi.

9 Maana nadhani ya ku wa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia na malaika na wana Adamu.

10 Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.

11 Hatta saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa makofi, hatuna makao;

12 tena twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twavumilia;

13 tukisingiziwa twasihi: tumefanywa kama takataka za dunia, na kifusi cha vitu vyote hatta sasa.

14 Siyaandiki haya illi kuwatahayarisha, hali kuwaonya kama watoto niwapendao. Maana ijapokuwa mna waalimu elfu katika Kristo, illakini hamna baba wengi.

15 Maana mimi ndiye aliyewazaa katika Kristo Yesu kwa Injili.

16 Bassi, nawasihini, mwe wafuasi wangu.

17 Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa.

18 Wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu.

19 Lakini nitakuja kwemi upesi, Bwana akipenda, nami nitajua, si neno lao waliojivuna, bali nguvu zao.

20 Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, hali katika nguvu.

21 Mnataka nini? Nije kwenu na fimbo, au katika upendo na roho ya upole?

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo