Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NA mimi, ndugu, sikuweza kunena nanyi kama na watu wenye tabia za rohoni, bali kama na watu wenye tabia za mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.

2 Nimewanywesha maziwa, sikuwalisha chakula; kwa maana mlikuwa hamjakiweza; naam, hatta sasa hamkiwezi, kwa maana hatta sasa m watu wa tabia za mwilini.

3 Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu.

4 Maana hapo mtu mmoja anenapo, Mimi ni wa Paolo; na mwingine, Mimi ni wa Apolio, je! hamwi watu wa tabia za mwilini?

5 Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.

6 Mimi nilipanda, Apollo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.

7 Kama ni hivyo, apandae si kitu, wala atiae maji, bali Mungu akuzae.

8 Bassi yeye apandae, na yeye atiae maji ni kitu kimoja, na killa mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.

9 Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu.

10 Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, nimeuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini killa mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

11 Maana msingi wa namna nyingine hapana mtu awezae kuweka, illa ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo.

12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huu dhahabu au fedha au vitu vya thamani au miti au majani an manyasi,

13 kazi ya killa mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto utajaribu kazi ya killa mtu, ni wa namna gani.

14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.

15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata khasara; lakini yeye mwenyewe ataokolewa; lakini kule kuokolewa kama kwa moto.

16 Hamjui ya kuwa ninyi hekalu ya Mungu, na ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiiharibu hekalu ya Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu ya Mungu ni takatifu, ambayo ni ninyi.

18 Mtu asijidanganye nafsi yake: kama mtu akijiona kuwa mweuye hekima kati yeuu katika dunia hii, na awe mpumbavu, apate kuwa mwenye hekima.

19 Maana hekima ya dunia hii ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasae wenye hekima katika hila yao.

20 Na tena, Bwana anajua mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili.

21 Bassi, asijisifu mtu katika wana Adamu.

22 Kwa maana vyote ni vyenu; ikiwa ni Paolo, au Apollo, au Kefa, au dunia, au uzima, au mauti, au vile vilivyo sasa, au vile vitakavyokuwa,

23 vyote ni vyenu, na ninyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo