1 Wakorintho 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NAMI nilipokuja kwenu ndugu, sikuja niwakhubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. 2 Maana naliazimu nisijue neno kwenu illa Yesu Kristo, nae amesulibiwa. 3 Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na khofu na matetemeko mengi. 4 Na neno langu na kukhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima ya kibinadamu yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho zenye nguvu, 5 imani yenu isiwe katika hekima ya wana Adamu, bali katika nguvu za Mungu. 6 Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa; 7 bali twanena hekima ya Mungu katika fumbo, ile iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu asili, kwa utukufu wetu; 8 ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu; 9 lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, Wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu, Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho yake. Maana Roho huchunguza yote, hatta mafumbo ya Mungu. 11 Maana ni nani ayajuae mambo ya bin Adamu illa roho ya bin Adamu iliyo ndani yake? Na vivyo hivyo mambo ya Mungu hakuna ayajuae illa Roho ya Mungu. 12 Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu. 13 Nayo twayanena, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali tuliyofimdishwa na Roho, tukiyalinganisha mamho ya rohoni na mambo va rohoni. 14 Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. 15 Lakini mtu wa rohoni huvatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. 16 Maana ni nani aliyejua nia ya Bwana, amwelemishe? Lakini sisi tuna nia ya Kristo. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania