Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA khabari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisaya Galatia, na ninyi fanyeni vivyo hivyo.

2 Siku ya kwanza ya juma killa mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; changizo zisifanyike hapo nitakapokuja:

3 nami nitakapofika nitawatuma wale mtakaowachagua kwa nyaraka, wachukue ihsani yenu hatta Yerusalemi.

4 Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.

5 Lakini nitakuja kwenu, nikipita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia.

6 Labda nitakaa kwenu; naam, labda nitashinda kwenu wakati wa baridi, mpate kunisafirisha wakati uwao wote nitakapokwenda.

7 Maana sitaki kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraja kukaa kwenu mda wa kitambo, Bwana akinijalia.

8 Lakini nitakaa katika Efeso mpaka Pentekote;

9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wengi wako wanipingao.

10 Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo khofu; maana anaifanya kazi ya Bwana kama mimi nami:

11 bassi mtu aliye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, illi aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu.

12 Lakini kwa khabari za Apollo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja nao ndugu, nae hakupenda kabisa kwenda sasa; lakini atakwenda sitakupopata nafasi.

13 Kesheni, simameni imara katika Imani, mwe waume, mwe hodari.

14 Mambo yenu yote yatendeke katika upendo.

15 Tena nawasihi, ndugu, (mnaijua nyumba ya Stefano kwamba ni malimbuko ya Akaia, nao wamejitia katika kazi ya kuwakhudumu watakatifu),

16 bassi watiini watu kama hawa, na killa mtu afanyae kazi pamoja nao, na kujitaabisha.

17 Nami nafurahi, kwa sababu ya kuwako kwao Stefano na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikarimia kwa wingi nilivopungukiwa kwenu.

18 Maana wamenihurudisha roho yangu, na roho zenu pia; bassi wajueni sana watu kama hao.

19 Makanisa ya Asia wawasalimu. Akula na Priskilla wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililo ndani ya nyumba yao.

20 Ndugu wote wawasalimu. Kasalimianeni kwa busu takatifu.

21 Hii ni salamu yangu mimi Paolo kwa nikono wangu mwenyewe.

22 Mtu aliye yote asiyempenda Bwana Yesu Kristo, na awe anathema. Maranatha.

23 Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

24 Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo