Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NAWAARIFU, ndugu, injili niliyowakhubirieni; ndiyo mliyoipokea, katika hiyo mnasimama,

2 na kwa hiyo mnaokolewa, ikiwa mnayashika sana maneno niliyowakhuhirieni; isipokuwa mliamini burre.

3 Kwa maana naliwapasha khabari ya mambo niliyoyapokea, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;

4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;

5 na ya kuwa alionekana na Kefa; tena na wathenashara;

6 baadae alionekana na ndugu zaidi ya khamsi mia pamoja; katika hao walio wengi wanaishi hatta sasa, wengine wamelala;

7 baadae alionekana na Yakobo; tena na mitume wote;

8 na mwisho wa watu wote, alionekana na mimi, kama nae aliyezaliwa si kwa wakati wake.

9 Maana mimi mdogo katika mitume, nisiyestahili kutajwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.

10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami.

11 Bassi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tukhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.

12 Bassi, ikiwa Kristo amekhubiriwa kwenu ya kwamba amefufuka, mbona wengine wenu wasema kwamba hakuna kiyama ya wafu?

13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo nae hakufufuliwa:

14 tena kama Kristo hakufufuliwa, bassi, kukhubiri kwetu ni burre na imani yenu ni burre.

15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uwongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambae hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo nae hakufufuliwa.

17 Na kama Kristo hakufufuliwa, imani yenu ni burre; mngali katika dhambi zenu.

18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.

19 Kama katika maisha haya tu tumemtumainia Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.

20 Lakini sasa Kristo amefufuka, limbuko lao waliolala.

21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.

22 Kwa kuwa katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.

23 Lakini killa mmoja mahali pake; limbuko Kristo; baadae walio wake Kristo, atakapokuja.

24 Ndipo palipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

25 Maana sharti amiliki yeye, hatta awaweke maadui wote chini ya miguu yake.

26 Adui wa mwisho atakaebatilishwa ni mauti.

27 Kwa kuwa alitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini akisema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hamo.

28 Bassi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe nae atatiishwa chini yake aliyemtiishia vitu vyote, illi Mungu awe yote katika yote.

29 Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje, bassi, kama wafu hawafufuki?

30 Kwa nini wakabatizwa kwa ajili yao? Na sisi, kwa nini tumo khatarini killa saa?

31 Naam, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa killa siku.

32 Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na nyama wakali kule Efeso, nina faida gani wasipofufuka wafu? Tule, tukanywe, maana kesho tutakufa.

33 Msidanganyike: mazumgumzo mabaya huharibu tabia njema.

34 Erevukeui kama ipasavyo, wala insiteude dhambi; kwa maana wengine hawamfahamu Mungu. Ninasema haya niwafedheheshe.

35 Labda mtu atasema, Wafufukaje wafu? Na kwa mwili gani waja?

36 Mpumbavu! uipandayo wewe haihuiki, isipokufa;

37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, illa punje tupu, ikiwa ya nganu au nyingineyo;

38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na killa mbegu mwili wake.

39 Nyama yote si nyama moja; bali nyingine ya wana Adamu, nyingine ya ngʼombe, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.

40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fakhari yake ya mbingu ni mbali, na fakhari yake ya duniani mbali.

41 Fakhari ya jua mbali, na fakhari ya mwezi mbali, na fakhari ya nyota mbali; maana iko tofauti ya fakhari kati ya nyota na nyota.

42 Kadhalika na kiyama ya wafu. Hupandwa katika nharibifu; hufufuka pasipo nharibifu;

43 hupandwa katika aibu; hufufuka katika fakhari; hupandwa katika udhaifu; hufufuka katika nguvu;

44 hupandwa mwili wa asili; hufufuka mwili wa roho. Ikiwa upo mwili wa asili, na wa roho upo.

45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza Adamu alikuwa nafsi hayi; Adamu wa mwisho roho yenye kuhuisha.

46 Lakini hautangulii wa roho, bali wa asili; baadae huja wa roho.

47 Mtu wa kwanza atoka katika inchi, wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.

48 Alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.

49 Na kama tulivyoichukua sura yake wa udongo, kadhalika tulaichukua sura yake wa mbinguni.

50 Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika.

51 Angalieni, nawaambieni siri; hatutalala wote, lakini wote tutabadilika,

52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa panda la mwisho; maana panda litalia, na wafu watafufuka, wasiwe na uharibifu, na sisi tutahadilika.

53 Maana sharti huu wenye uharibifu uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

54 Bassi, uharibifu huu utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.

55 U wapi, mauti, uchungu wako? Ku wapi, kaburi, kushinda kwako?

56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni sharia.

57 Lakini tumshukuru Mungu atupae kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

58 Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo