Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu.

2 Maana yeye anenae kwa lugha, haneni na watu, bali na Mungu; maana hapana asikiae; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

3 Bali yeye akhutubuye, anena na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.

4 Anenae kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali akhutubuye hulijenga Kanisa.

5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kukhutubu; maana yeye akhutubuye ni mkuu kuliko yeye anenae kwa lugha, isipokuwa afasiri, illi kusudi Kanisa lipate kujengwa.

6 Bassi, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nanena nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya khotuba, au kwa njia ya fundisho?

7 Hatta vitu visivyo na uhayi vitoapo sauti, ikiwa filimbi, ikiwa kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi?

8 Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana, nani atakaejifanya tayari kwa vita?

9 Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ile lugha neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana nitakuwa mkinena katika hewa tu.

10 Yumkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hapana moja isiyo na maana.

11 Bassi nisipojua maana ya ile sauti nitakuwa mshenzi kwake yeye anenae; nae atakuwa mshenzi kwangu.

12 Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni mzidi sana kuwa nazo illi kulijenga Kanisa.

13 Kwa hiyo yeye anenae kwa lugha na aombe apewe kufasiri.

14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazizai matunda.

15 Imekuwaje, bassi? Nitaomba kwa roho, na nitaomba kwa akili; nitaimba kwa roho, na nitaimba kwa akili.

16 Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika daraja ya mjinga ataitikaje, Amin, baada ya kushukuru kwako, nae hayajui usemayo?

17 Maana ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi.

18 Namshukuru Mungu wangu, nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote;

19 lakini napenda kunena maneno matano katika kanisa kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno elfu kumi kwa lugha.

20 Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.

21 Imeandikwa katika torati ya kama, Nitanena na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, na hatta hivi hawatanisikia, asema Bwana.

22 Bassi, lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini. Lakini kukhutuhu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.

23 Bassi ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wananena kwa lugha, kiisha wakaingia watu wajinga au wasioamini, je! hawatasema ya kwamba mna wazimu?

24 Lakini wote wakikhutubu, akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, alaumiwa na wote, ahukumiwa na wote;

25 na hivyo siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo, akianguka kifudifudi, atamwabudu Mungu, akikiri ya kuwa Mungu yu kati yenu hila shaka.

26 Imekuwaje bassi, ndugu? Mkutanapo pamoja, killa mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana lugha, ana ufunuo, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.

27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja afasiri.

28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; anene na nafsi yake au na Mungu.

29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapamhanue.

30 Lakini mwingine aliyeketi, akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.

31 Kwa maana nyote mwaweza kukhutubu mmoja mmoja, illi wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.

32 Na roho za manabii huwatii manabii.

33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.

34 Wanawake wanyamaze katika kanisa, maana hawana rukhusa kunena; bali watii, kama vile inenavyo sharia nayo.

35 Na wakitaka kujifunza neno, na waulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu, wanawake kunena katika kanisa.

36 Je! neno la Mungu limetoka kwenu tu? au limewafikia ninyi peke yenu?

37 Mtu akijiona kuwa nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue haya ninayowaandikieni, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.

38 Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.

39 Kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kukhutubu, wala msikataze kunena kwa lugha.

40 Mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratihu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo