1 Wakorintho 13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NIJAPOSEMA kwa lugha za wana Adamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upato uvumao. 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi. 3 Tena mkiwagawia maskini mali yangu yote, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4 Upendo husubiri, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni, 5 haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 hustahimili yote, huamini yote, hutumaini yote, huvumilia yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. 9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; 10 lakini ijapo iliyo kamili, iliyo kwa, sehemu itabatilika. 11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. 12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso: wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana. 13 Bassi, sasa inabaki imani, tumaini, upendo, hizi tatu; na iliyo kuu katika hizi ni upendo. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania