Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 MWE wafuasi wangu kama mimi nilivyo mfuasi wa Kristo.

2 Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.

3 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha killa mwanamume ni Kristo na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

4 Killa mwanamume, asalipo, au atoapo unabii, nae ana kitu kichwani, yuaibisha kichwa chake.

5 Bali killa mwanamke asalipo, au atoapo unabii, bila kufunika kichwa chake, yuaibisha kichwa chake; kwa maana yu sawa sawa nae aliyekata nywele zake.

6 Maana mwanamke asipofunikwa na anyoe. Au ikiwa ni unyonge mwanamke akate nywele zake au kunyoa, na afunikwe.

7 Kwa maana haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanake ni utukufu wa mwanamume.

8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.

9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.

10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani pake, kwa ajili ya malaika.

11 Illakini mwanamume hawi pasipo mwanamke, wala mwanamke pasipo mwanamume, katika Bwana.

12 Maana kama vile mwanamke alitoka katika mwanamume, vivyo hivyo mwanamume nae huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu.

13 Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu. Je! inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa chake?

14 Je! sharia ya asili yenyewe haiwafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake;

15 lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni ntukufu kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu illi ziwe badala ya mavazi.

16 Lakini mtu aliye yote, akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.

17 Katika kuagiza hayo, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa khasara;

18 kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; na nussu kidogo nasadiki:

19 kwa maana lazima kuwapo uzushi kwenu, illi waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.

20 Bassi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana;

21 kwa maana killa mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hatta huyu ana njaa, na huyu amelewa.

22 Je! hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau Kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha wasio na kitu? Niwaambieni? niwasifu kwa haya? Siwasifu.

23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowakhubirini, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,

24 na akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangii.

25 Vivi hivi nacho kikombe baada ya kula, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu: fanyeni liivi killa mnywapo, kwa ukumbusho wangu.

26 Maana killa mwulapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hatta ajapo.

27 Bassi killa aulae mkate huu, au kunywea kikombe hiki, asivyostahili, atakuwa amejipatia khatiya kwa ajili ya mwili na damu ya Bwana.

28 Lakini mtu ajihoji nafsi yake, ndivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

29 Maana alae na kunywa asivyostahili, hula na hunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua mwili wa Bwana.

30 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.

31 Lakini tukijihukumu vema nafsi zetu, tusingehukumiwa.

32 Tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, tusipate kupasishwa adhabu pamoja na dunia.

33 Bassi, ndugu zangu, mkutanikapo mpate kula, mngojane;

34 mtu akiwa na njaa, ale nyumbani; msipate kukutanika kwa hukumu. Nayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo