Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Wakorintho 10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NDUGU, sitaki mkose kufahamu ya kuwa baba zetu wote walikuwa chini ya wingu, wote wakapita kati ya bahari;

2 wote wakabatizwa kwa Musa katika wingu na katika bahari;

3 wote wakala chakula kile kile cha roho;

4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho: kwa maana walikunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ni Kristo.

5 Lakini walio wengi, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.

6 Haya yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu ya kutamani mabaya, kama wale walivyotamani.

7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama wacheze.

8 Wala tusifanye uasharati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka muda wa siku moja watu ishirini na tatu elfu.

9 Wala tusimjaribii Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.

10 Wala msinungʼunike, kama wengine wao walivyommgʼunika, wakaharibiwa na mharabu.

11 Haya yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa illi kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

12 Bassi anaejidhani amesimama aangalie asianguke.

13 Jaribu halikuwapata ninyi, illa ya kadiri ya kibinadamu; na Mungu yu amini; hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, illi mweze kustahimili.

14 Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.

15 Nasema kama nti watu wenye akili; ufikirini ninyi ninenalo.

16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule timmegao, si ushirika wa mwili wti Kristo?

17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.

18 Waangalieni Israeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! hawana shirika na madhbahu?

19 Bassi niseme nini? ya kwamba sanamu ni kitu? au ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu?

20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo mataifi, wavitolea mashetani, wala si Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani.

21 Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

22 Au twamtia Bwana wivu? au tuna nguvu zaidi ya yeye?

23 Vitu vyote ni halali kwangu; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali kwangu; hali si vitu vyote vijengavyo.

24 Mtu asitafute kujifaidia nafsi yake, bali kumfaidia mwenzake.

25 Killa kitu kiuzwacho sokoni kulani, bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri;

26 maana dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.

27 Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kulani killa kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri.

28 Lakini mtu akiwaambieni, Kitu hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu, msile, kwa ajili yake yeye aliyekuonyesha, na kwa ajili ya dhamiri; maana dunia ni mali ya Bwana na vitu vyote viijazavyo.

29 Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?

30 Na nikitumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho?

31 Bassi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

32 Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunaui wala Kanisa la Mungu:

33 vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, bali faida yao walio wengi, wapafe kuokolewa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo