1 Wakorintho 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 PAOLO, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, 2 kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu: 3 Neema na iwe kwenu, na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. 4 Namshukuru Mungu wangu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; 5 kwa kuwa katika killa jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; 6 kama ushuhuda wa Kristo ulivyothubutika kwenu; 7 hatta hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 8 na yeye atawathubutisheni hatta mwisho, msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Mungu ni mwaminifu, ambae mliitwa nae muingie katika ushirika wa Mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu. 10 Nawasihi ninyi, ndugu, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mnene nyote mamoja, pasiwe kwenu faraka, bali mwe mmekhitimu katika nia moja na shauri moja. 11 Kwa maana nimearifiwa khabari zenu, ndugu, na wale walio wa nyumba ya Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. 12 Bassi, nasema neno hili, ya kwamba killa mtu wa kwenu husema, Mimi wa Paolo, na mimi wa Apollo, na mimi wa Kefa, na mimi wa Kristo. 13 Je! Kristo amegawanyika? Paolo alisulibiwa kwa ajili yenu? 14 An mlibatizwa kwa jina la Paolo? 15 Namshukuru Mungu, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, illa Krispo na Gayo; mtu asije akasema kwamba nimebatiza kwa jina langu mwenyewe. 16 Tena nalibatiza watu wa nyumba ya Stefano; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu mwingine. 17 Maana Kristo hakunituma illi nibatize, bali niikhubiri Injili; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo nsije nkabatilika. 18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19 Maana imeandikwa Nitaharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa. 20 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mleta hoja wa dunia bii? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia liii kuwa upumbavu? 21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa. 22 Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; 23 bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu, 24 bali kwao waitwao, Wayahudi na Wayunani pia, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. 25 Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wana Adamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wana Adamu. 26 Maana angalieni wito wenu, ndugu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo waliokwitwa; 27 bali Mungu aliyachagua mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena alivichagua vitu dhaifu vya dunia illi wenye nguvu waaibishwe; 28 nae alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, na vitu ambavyo haviko, illi avibatilishe vilivyoko; 29 mwenye mwili aliye yote asije akajisifu mbele ya Mungu. 30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi; 31 kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye ajisifuye ajisifu katika Bwana. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania