Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Timotheo 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 USIMKEMEE mzee, bali mwonye kama baba, na wadogo wako kama ndugu:

2 wanawake wazee kama mama, wanawake vijana kama ndugu, kwa utakatifu wote.

3 Waheshimu wajane walio wajane kweli kweli.

4 Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kutenda yaliyo wajib wao katika nyumba yao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Maana jambo hili ni zuri, tena lipendezalo mbele za Mungu.

5 Bali yeye aliye mjane kweli kweli, na kuachwa peke yake, amemwekea Mungu tumaini lake, nae hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.

6 Na yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hayi.

7 Uwaagize haya, illi wawe bawana lawama.

8 Lakini mtu asiyewatunza walio wake na khassa watu wa nyumba yake ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.

9 Mjane aandikwe, ikiwa umri wake amepata miaka sittini, isipungue, nae amekuwa mke wa mume mmoja,

10 na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.

11 Bali wajane walio vijana nkatae kuwaandika, maana wakiona tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa,

12 nao wana hukumu, kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza.

13 Na pamoja na hayo wajifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi, hujishughulisha na mambo ya wengine wakinena maneno yasiyowapasa.

14 Bassi napenda wajane wasio wazee waolewe, wazae watoto, watawale mambo ya nyumbani, wasimpe adui nafasi ya kulaumu;

15 maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.

16 Mwanamume au mwanamke aamimye, akiwa na wajane, awasaidie, kanisa lisilemewe; illi liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.

17 Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.

18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ngʼombe apurapo nganu: na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.

19 Usikubali mashitaka juu ya mzee, illa kwa vinywa vyao mashahidi wawili au watatu.

20 Wale watendao dhambi, uwakemee mbele ya watu wote, illi na wengine waogope.

21 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.

22 Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usishiriki dhambi za watu wengine.

23 Jilinde nafsi yako uwe safi; tokea sasa usinywe maji tu, bali tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo marra nyingi.

24 Dhambi za watu wengine ni dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhamhi zao zawafuata.

25 Vivyo hivyo matendo mazuri ni dhahiri; na yale yasiyo dhahiri hayawezi kusetiriwa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo