1 Timotheo 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 ROHO yanena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho watu watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani, 2 kwa unafiki wa watu wasemao uwongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru kujiepusha na vyakula ambavyo Mungu aliviumba vopokewe kwa shukrani na walio na imani na wenye kuijua sana kweli. 4 Kwa maana killa kiumhe cha Mungu ni kizuri, waki hakuma cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani: 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kuomba. 6 Ukiwakumhusha ndugu hayo, utakuwa mkhudumu mwema wa Yesu Kristo, na mzoevu wa maneno ya imani, na ya mafundisho yale mazuri uliyoyafuata. 7 Bali hadithi za kizee, zisizo za dini, uzikatae. 8 Jitahidi kupata utawa. Maana, kujitahidi kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, hali utawa hufaa kwa mambo yote; maana nna ahadi ya uzima wa sasa na wa ule utakaokuwa. 9 Neno hili ni amini, lastahili kukubaliwa na wote. 10 Kwa maana twajitaabisha na kujitahidi katika jambo hili, kwa sababu twamtumaini Mungu aliye hayi aliye mwokozi wa watu wote, khassa wa hao waaminio. 11 Uwaagize watu hayo na kuwafundisha hayo. 12 Mtu asiudharau ujana wako, bali uwe mfano kwao waaminio, katika usemi, na katika mwenendo, na katika upendo, na katika imani, na katika utakatifu. 13 Hatta nijapo, fanya bidii katika kusoma na kuonya ua kufundisha. 14 Usiache kuitumia ile karama iliyo udani yako uliyopewa wewe kwa unabii, na kwa kuwekewa mikono ya wazee. 15 Uyatafakari hayo, ukae katika hayo. Kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. 16 Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania