Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Timotheo 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, kabla ya mambo yote, dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

2 kwa ajili ya wafalme, na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya ntulivu na amani, katika utawa wote, na ustahifu.

3 Maana hili ni zuri, lenye kibali mbele za Mwokozi wetu Mungu

4 atakae watu wote waokolewe wakapate kujua sana yaliyo kweli.

5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wana Adamu ni mmoja, mwana Adamu, Kristo Yesu,

6 aliyejitoa nafsi yake kuwa ukombozi kwa ajili ya wote utakaoshuhudiwa kwa majira yake;

7 kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.

8 Bassi nataka wanaume waombe killa mahali, wakimua mikono mitakatifu, pasipo hasira na majadiliano.

9 Na vivyo hivyo wanawake wajipambe kwa mavazi ya kujisetiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi, si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

10 bali kama iwapasavyo wanawake wanaokiri utawa, kwa matendo mema.

11 Mwanamke na ajifunze kalika utulivu, akitii kwa killa namna.

12 Simpi mwanamke rukhusa kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali kuwa katika utulivu.

13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadae.

14 Na Adamu hakudanganywa, bali mwanamke akidanganywa aliingia hali ya kukosa.

15 Lakini ataokolewa, kwa ule uzazi, kama wakidumu katika imani na npendo na utakatifu pamoja na moyo wa kiasi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo