Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Timotheo 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu;

2 kwa Timotheo, mwana wangu khassa katika imani, Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

3 Kama vile nilivyotaka ukae katika Efeso nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, illi, nwaagize wengine wasifundishe elimu ya namna nyingine,

4 wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si ujenzi wa Mungu ulio katika imani; bassi sasa nakuagiza vivyo hivyo.

5 Bali kusudi la mausia hayo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki:

6 wengine wakikosa bayo wamepotea, wakigeukia maneno ya ubatili;

7 wapenda kuwa waalimu wa sharia, wasiyafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa utbabiti.

8 Lakini twajua ya kuwa sharia ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia ya kisharia;

9 nawe ufahamu neno hili, ya kuwa sharia haimkhusu mtu wa haki, bali maasi, mi wasio taratihu, na makafiri, na wenye dhambi, na wasio watakatifu, na wasiomcha Mungu, na wauao baba zao, na wauao mama zao, mi wauaji,

10 na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na wawongo, mi waapao uwongo, na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

11 kama vile ilivyonenwa katika injili ya utukufu wa Mungu ahimidiwae, niliyoaminiwa mimi.

12 Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akiniweka katika khuduma yake;

13 mimi niliyekuwa kwanza mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri: lakini nalirehemiwa kwa kuwa nalitenda hivyo kwa njinga, na kwa kutokuwa na imani;

14 na neema ya Bwana wetu ilizidi sana pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.

15 Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.

16 Lakini kwa sababu hii nalirehemiwa, illi katika mimi, wa kwanza, Yesu Kristo adhihirishe uvumilivu wote, niwe mfano kwa wale watakaomwamini baadae, wapate uzima wa milele.

17 Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.

18 Agizo hilo nakupa iwe akiba, mwanangu Timotheo, kwa ajili ya maneno ya unabii yalivotangulia juu yako, illi katika hayo ufanye vile vita vizuri;

19 nwe mwenye imani na dhamiri njema; wengine wamezisukumia mbali hizo, wakavunja chombo cha imani.

20 Katika hao wamo Humenayo na Iskander, ambao nimempa Shetani wafundishwe wasimtukane Mungu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo