1 Petro 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KADHALIKA ninyi wake, watumikieni waume o zenu; kusudi, ikiwa wako waume wasioliamini Neno, kwa mwenendo wa wake zao, pasipo Neno lile, wavutwe; 2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa khofu. 3 Kujipamba kwao, kusiwe kujipamba kwa nje, ndio kusuka nywele, na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4 bali mtu wa moyoni asiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5 Maana bivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumainia Mungu, wakiwatumikia waume zao; 6 kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; ninyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala kushitushwa kwa khofu yo yote. 7 Ninyi wanme kadhalika, kaeni na wake zenu kwa akili; mkimpa mke heshima, kama chombo kisieho nguvu, na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi sala zenu zisizuiliwe. 8 Neno la mwisbo ni hili; mwe na nia moja, wahurumianao, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; 9 watu wasiolipa baya badala ya baya, au laumu badala ya laumu; bali wabarikio; kwa sababu ndiyo mlioitiwa illi mrithi baraka. 10 Kwa maana, Atakae kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie nlimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila: 11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. 12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombo yao: Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya. 13 Na ni nani atakaewadhuru, mkiwa waigaji wa wema? 14 Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, in kheri; msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; 15 bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu; mwe tayari siku zote kumjibu killa mtu akuulizae khabari za tumaini lililo ndani yenu; kwa upole na kwa khofu, 16 mkiwa na dhamiri njema, illi katika neno lile mnalosingiziwa kwamba m watenda mabaya, wataha yarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. 17 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndio mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya. 18 Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa. 19 Kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, 20 akawakhubiri watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ndani yake watu wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 21 Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo; 22 alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania