Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Petro 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, mkiwekea mbali uovu wote na hila yote na unafiki na husuda na niasingizio yote,

2 kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu;

3 ikiwa mmeonja kwamba Bwana ni mwenye fadhili.

4 Mkimwendea yeye, jiwe lililo hayi, lililokataliwa na wana Adamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye thamani,

5 ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.

6 Kwa kuwa ndiyo yaliyomo katika maandiko, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye thamani, Na killa amwaminiye hatatabayarika.

7 Bassi, thamani hii ni kwenu ninyi mnaoamini, bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni;

8 tena, Jiwe lakujikwaza mguu, na mwamba wa kujiangusha; maana hujikwaza kwa neno lile, wakiliasi, nao waliwekwa wapate hayo.

9 Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

11 Mapenzi, nakusihini kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho;

12 mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.

13 Tumikieni killa kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa mfalme, kama mwenye cheo kikuliwa;

14 ikiwa wakubwa, kama wanaotumwa nae kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema;

15 kwa sababu ndio mapenzi ya Mungu, kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;

16 kama huru, na wasiontumia uhuru kwa kusetiri ubaya, bali kaina watumwa wa Mungu.

17 Heshimuni walu wote. Upendeni udugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

18 Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa khofu nyingi; sio wao walio wema na wenye upole fu, bali nao walio wakali.

19 Maana huu ndio wema khassa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, ateswapo isivyo baki.

20 Kwa maana ni sifa gani kuvumilia, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kuvumilia, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema khassa mbele za Mungu.

21 Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo nae aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake;

22 yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake;

23 yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki;

24 yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa.

25 Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo