1 Petro 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 PETRO, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Mtawanyiko, wakaao bali ya wageni katika Ponto, Galatia, Kappadokia, Asia na Bithunia, 2 kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu. 3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo, 4 tupate urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu, 5 mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. 6 Mnafurahi sana kwa ajili yake, ijapokuwa sasa kwa kitambo, ikiwa ni lazima, mmchuzunishwa kwa majaribu ya namna mbali mbali, 7 illi kujaribiwa kwake imani yenu, ambako kuna thamani kuu kuliko dbahabu ipoteayo, ijapokuwa imejaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo: 8 ambae mwampenda, ijapokuwa hamkumwona: ambae ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini, na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, iliyotukuzwa, 9 mkiupokea mwisho wa imani yenu, wokofu wa roho zenu. 10 Katika khabari ya wokofu huo walitafutatafuta na kuchunguzachunguza manabii waliotabiri khabari va neema itakayowafikia, 11 wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo. 12 Waliofunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walitumika katika mambo hayo, ambayo sasa yamekhubiriwa kwenu na wale waliowakhubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hiayo malaika wanatamani kuyachuugulia. 13 Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, mwe na kiasi, kwa utimilifu mkiitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza, za ujinga wenu; 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi mwe watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16 maana imeandikwa, Mwe watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 17 Na ikiwa mnamwita Baba yeye ahukumuye killa mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa khofu kafika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni; 18 mkijua kwamba hamkukombolewa kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu, mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlionpokea kwa baba zenu; 19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo, 20 aliyejuliwa tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifimuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu, 21 ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu. 22 Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo; 23 kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele. 24 Maana, Mwili wote kama majani, Na utukufu wake wote kama ua la majaui. Majani hukauka na ua lake huanguka; 25 Bali Neno la Bwana hudumu hatta milele. Na neno bilo ni neno lile jema lililokhubiriwa kwenu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania