wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.
Zekaria 8:18 - Swahili Revised Union Version Tena neno la BWANA wa majeshi likanijia, kusema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Neno la Mwenyezi-Mungu wa majeshi lilinijia mimi Zekaria: Biblia Habari Njema - BHND Neno la Mwenyezi-Mungu wa majeshi lilinijia mimi Zekaria: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Neno la Mwenyezi-Mungu wa majeshi lilinijia mimi Zekaria: Neno: Bibilia Takatifu Neno la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni likanijia tena. Neno: Maandiko Matakatifu Neno la bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia tena. BIBLIA KISWAHILI Tena neno la BWANA wa majeshi likanijia, kusema, |
wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.
BWANA wa majeshi asema hivi, Saumu ya mwezi wa nne, na saumu ya mwezi wa tano, na saumu ya mwezi wa saba, na saumu ya mwezi wa kumi, zitakuwa furaha na shangwe, na sikukuu za kuchangamkia, kwa nyumba ya Yuda; basi zipendeni kweli na amani.
BWANA wa majeshi asema hivi, Mikono yenu na iwe hodari, ninyi mnaosikia siku hizi maneno haya kwa vinywa vya manabii, waliokuwapo siku hiyo ulipowekwa msingi wa nyumba ya BWANA wa majeshi; yaani, hekalu hilo; ili lijengwe.
Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.
Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.