Zaburi 2:1 - Swahili Revised Union Version Mbona mataifa yanafanya ghasia, Na watu kuwaza mambo ya bure? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa nini mataifa yanafanya ghasia? Mbona watu wanafanya njama za bure? Biblia Habari Njema - BHND Kwa nini mataifa yanafanya ghasia? Mbona watu wanafanya njama za bure? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa nini mataifa yanafanya ghasia? Mbona watu wanafanya njama za bure? Neno: Bibilia Takatifu Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na makabila ya watu kula njama bure? Neno: Maandiko Matakatifu Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure? BIBLIA KISWAHILI Mbona mataifa yanafanya ghasia, Na watu kuwaza mambo ya bure? |
Ungameni pamoja, enyi makabila ya watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande.
Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.
Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate;
Makutano wote wakaondoka wakawaendea, mahakimu wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.
Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.