Zaburi 13:5 - Swahili Revised Union Version Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mimi nazitumainia fadhili zako; moyo wangu na ufurahie wokovu wako. Biblia Habari Njema - BHND Lakini mimi nazitumainia fadhili zako; moyo wangu na ufurahie wokovu wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mimi nazitumainia fadhili zako; moyo wangu na ufurahie wokovu wako. Neno: Bibilia Takatifu Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako. BIBLIA KISWAHILI Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako. |
Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako.
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.
Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.
jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.
Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;