Na walipotoka mjini, kabla hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema?
Zaburi 109:5 - Swahili Revised Union Version Wamenilipa mabaya kwa mema yangu, Na chuki badala ya upendo wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wananilipa uovu kwa wema wangu, na chuki kwa mapendo yangu. Biblia Habari Njema - BHND Wananilipa uovu kwa wema wangu, na chuki kwa mapendo yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wananilipa uovu kwa wema wangu, na chuki kwa mapendo yangu. Neno: Bibilia Takatifu Wananilipiza mabaya kwa mema, chuki badala ya urafiki wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Wananilipiza mabaya kwa mema, chuki badala ya urafiki wangu. BIBLIA KISWAHILI Wamenilipa mabaya kwa mema yangu, Na chuki badala ya upendo wangu. |
Na walipotoka mjini, kabla hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema?
Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.
Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
Je! Mabaya yalipwe badala ya mema? Maana wameichimbia nafsi yangu shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele zako, ili niseme mema kwa ajili yao, nikaigeuze ghadhabu yako isiwapate.
Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.
Kwa kuwa alihatarisha maisha yake, na kumpiga yule Mfilisti, naye BWANA akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure?