Nawe uliipasua bahari mbele yao, hata wakapita katikati ya bahari katika nchi kavu; na wale waliokuwa wakiwafuatia ukawatupa vilindini, kama jiwe katika maji makuu.
Yoshua 24:6 - Swahili Revised Union Version Nikawatoa baba zenu watoke Misri; nanyi mkaifikia bahari; Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka Bahari ya Shamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Niliwatoa wazee wenu kutoka Misri na kuwaleta hadi kwenye bahari ya Shamu. Wamisri waliwafuatia wakiwa na magari na askari wapandafarasi. Biblia Habari Njema - BHND Niliwatoa wazee wenu kutoka Misri na kuwaleta hadi kwenye bahari ya Shamu. Wamisri waliwafuatia wakiwa na magari na askari wapandafarasi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Niliwatoa wazee wenu kutoka Misri na kuwaleta hadi kwenye bahari ya Shamu. Wamisri waliwafuatia wakiwa na magari na askari wapandafarasi. Neno: Bibilia Takatifu Nilipowatoa baba zenu Misri, mlifika kwenye bahari, nao Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari ya vita na wapanda farasi hadi Bahari ya Shamu. Neno: Maandiko Matakatifu Nilipowatoa baba zenu Misri, mlifika kwenye bahari, nao Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka kwenye Bahari ya Shamu. BIBLIA KISWAHILI Nikawatoa baba zenu watoke Misri; nanyi mkaifikia bahari; Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka Bahari ya Shamu. |
Nawe uliipasua bahari mbele yao, hata wakapita katikati ya bahari katika nchi kavu; na wale waliokuwa wakiwafuatia ukawatupa vilindini, kama jiwe katika maji makuu.
Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu elfu mia sita wanaume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto.
Ilikuwa siku ile ile moja, BWANA akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.
Kwa maana nilikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami niliwatuma Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako.
Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika Bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arubaini.
Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa.