Yona 4:1 - Swahili Revised Union Version Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini jambo hilo halikumpendeza Yona hata kidogo, akakasirika sana. Biblia Habari Njema - BHND Lakini jambo hilo halikumpendeza Yona hata kidogo, akakasirika sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini jambo hilo halikumpendeza Yona hata kidogo, akakasirika sana. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. BIBLIA KISWAHILI Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika. |
Mungu akamwambia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa.
Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?
Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.
Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona ninyi wenyewe kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.