Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
Yohana 8:45 - Swahili Revised Union Version Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi nasema ukweli, na ndiyo maana nyinyi hamniamini. Biblia Habari Njema - BHND Mimi nasema ukweli, na ndiyo maana nyinyi hamniamini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi nasema ukweli, na ndiyo maana nyinyi hamniamini. Neno: Bibilia Takatifu Lakini kwa sababu nimewaambia kweli, hamkuniamini! Neno: Maandiko Matakatifu Lakini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini! BIBLIA KISWAHILI Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki. |
Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.
Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?
na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.