Yohana 8:36 - Swahili Revised Union Version Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli. Biblia Habari Njema - BHND Mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli. BIBLIA KISWAHILI Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. |
Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.
Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.