Akalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Yohana 4:13 - Swahili Revised Union Version Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamjibu, “Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena. Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamjibu, “Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamjibu, “Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena. Neno: Bibilia Takatifu Isa akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki, ataona kiu tena. BIBLIA KISWAHILI Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; |
Akalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
lakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.