Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)
Yohana 21:21 - Swahili Revised Union Version Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Petro alipomwona huyo, akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?” Biblia Habari Njema - BHND Basi, Petro alipomwona huyo, akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Petro alipomwona huyo, akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?” Neno: Bibilia Takatifu Petro alipomwona huyo mwanafunzi, akamuuliza Isa, “Bwana, na huyu je?” Neno: Maandiko Matakatifu Petro alipomwona huyo mwanafunzi, akamuuliza Isa, “Bwana, na huyu je?” BIBLIA KISWAHILI Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je? |
Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)
Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nitakapokuja, imekuhusuje wewe? Wewe unifuate mimi.