Maneno yao yakaonekana kuwa kama upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro aliondoka akaenda mbio hadi kaburini, akainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu; akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia.
Yohana 20:3 - Swahili Revised Union Version Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini. Biblia Habari Njema - BHND Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini. Neno: Bibilia Takatifu Petro na yule mwanafunzi mwingine wakaondoka mara moja kuelekea kaburini. Neno: Maandiko Matakatifu Petro na yule mwanafunzi mwingine wakaondoka mara kuelekea kaburini. BIBLIA KISWAHILI Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini. |
Maneno yao yakaonekana kuwa kama upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro aliondoka akaenda mbio hadi kaburini, akainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu; akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia.
Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini.