Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yobu 9:3 - Swahili Revised Union Version

Kama akipenda kushindana naye, Hawezi kumjibu neno moja katika elfu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kama mtu angethubutu kushindana naye, hataweza kufika mbali; hata kujibu swali moja kati ya elfu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kama mtu angethubutu kushindana naye, hataweza kufika mbali; hata kujibu swali moja kati ya elfu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kama mtu angethubutu kushindana naye, hataweza kufika mbali; hata kujibu swali moja kati ya elfu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ingawa mtu angetaka kushindana naye, hangeweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ingawa mtu angetaka kushindana naye, asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kama akipenda kushindana naye, Hawezi kumjibu neno moja katika elfu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yobu 9:3
18 Marejeleo ya Msalaba  

Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa; Nijulishe kwa nini unapingana nami.


Yuko nani atakayeshindana nami? Maana sasa nitanyamaza kimya na kukata roho.


Kwa nini unapingana naye, ukisema, Hatajibu hata neno langu moja?


Kwani yeye hana haja ya kumfikiria mtu zaidi, ili aende mbele za Mungu ahukumiwe.


Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.


Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.


Je! Mimi nitamjibuje, Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye?


Ingawa mimi ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; Ingawa mimi ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa mimi ni mpotovu.


Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.


Kwa maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Nami nimevunjika moyo.


La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwa nini umeniumba hivi?


Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani yetu.


ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.