Yobu 7:4 - Swahili Revised Union Version Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilalapo nasema, ‘Nitaamka lini?’ Kwani saa za usiku huwa ndefu sana; nagaagaa kitandani mpaka kuche! Biblia Habari Njema - BHND Nilalapo nasema, ‘Nitaamka lini?’ Kwani saa za usiku huwa ndefu sana; nagaagaa kitandani mpaka kuche! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilalapo nasema, ‘Nitaamka lini?’ Kwani saa za usiku huwa ndefu sana; nagaagaa kitandani mpaka kuche! Neno: Bibilia Takatifu Nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’ Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’ Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko. BIBLIA KISWAHILI Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke. |
Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu, Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.
Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi.
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani, usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.
asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.