Yobu 21:4 - Swahili Revised Union Version Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, mimi namlalamikia binadamu? Ya nini basi, nikose uvumilivu? Biblia Habari Njema - BHND Je, mimi namlalamikia binadamu? Ya nini basi, nikose uvumilivu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, mimi namlalamikia binadamu? Ya nini basi, nikose uvumilivu? Neno: Bibilia Takatifu “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? Kwa nini nisikose subira? Neno: Maandiko Matakatifu “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? Kwa nini nisikose subira? BIBLIA KISWAHILI Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri? |
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa.