Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, na pia mambo yote ambayo mfalme amemfanikisha kwayo, na jinsi alivyompandisha cheo juu ya wakuu na watumishi wa mfalme.
Yobu 1:2 - Swahili Revised Union Version Kisha walizaliwa kwake watoto saba wa kiume, na binti watatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yobu alikuwa na watoto saba wa kiume na watatu wa kike; Biblia Habari Njema - BHND Yobu alikuwa na watoto saba wa kiume na watatu wa kike; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yobu alikuwa na watoto saba wa kiume na watatu wa kike; Neno: Bibilia Takatifu Alikuwa na wana saba na binti watatu, Neno: Maandiko Matakatifu Alikuwa na wana saba na binti watatu, BIBLIA KISWAHILI Kisha walizaliwa kwake watoto saba wa kiume, na binti watatu. |
Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, na pia mambo yote ambayo mfalme amemfanikisha kwayo, na jinsi alivyompandisha cheo juu ya wakuu na watumishi wa mfalme.
Kisha BWANA akamrejeshea Ayubu mali yake, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.
Basi hivyo BWANA akaubariki huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu moja, na punda wake elfu moja.
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.