Katika siku zake, Farao Neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana na mfalme wa Ashuru, akafika mto Frati; naye mfalme Yosia akaenda kupigana naye; naye mfalme wa Misri akamwua huko Megido, hapo alipoonana naye.
Yeremia 22:12 - Swahili Revised Union Version bali katika mahali pale walipomchukua mateka ndipo atakapokufa, wala hataiona nchi hii tena kamwe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema bali atafia hukohuko walikomchukua utumwani. Kamwe hataiona tena nchi hii. Biblia Habari Njema - BHND bali atafia hukohuko walikomchukua utumwani. Kamwe hataiona tena nchi hii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza bali atafia hukohuko walikomchukua utumwani. Kamwe hataiona tena nchi hii.” Neno: Bibilia Takatifu Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.” Neno: Maandiko Matakatifu Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.” BIBLIA KISWAHILI bali katika mahali pale walipomchukua mateka ndipo atakapokufa, wala hataiona nchi hii tena kamwe. |
Katika siku zake, Farao Neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana na mfalme wa Ashuru, akafika mto Frati; naye mfalme Yosia akaenda kupigana naye; naye mfalme wa Misri akamwua huko Megido, hapo alipoonana naye.
Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia awe mfalme mahali pa Yosia babaye, akambadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu, lakini akamwondoa Yehoahazi; akaenda naye Misri, naye akafa huko.
Basi, BWANA asema hivi, kuhusu habari za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.
Maana BWANA wa majeshi Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama hasira yangu, na ghadhabu yangu, ilivyomwagwa juu ya hao wakaao Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu, mtakapoingia Misri; nanyi mtakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu; wala hamtapaona mahali hapa tena.