Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.
Yeremia 12:9 - Swahili Revised Union Version Je! Urithi wangu umekuwa kwangu kama ndege mwenye madoadoa? Ndege wakali wamemzunguka pande zote? Nendeni, wakusanyeni pamoja wanyama wote wa mwituni, waleteni ili wale. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wateule wangu wamekuwa ndege mzuri wanaoshambuliwa na kozi pande zote. Nenda ukawakusanye wanyama wote wakali waje kushiriki katika karamu. Biblia Habari Njema - BHND Wateule wangu wamekuwa ndege mzuri wanaoshambuliwa na kozi pande zote. Nenda ukawakusanye wanyama wote wakali waje kushiriki katika karamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wateule wangu wamekuwa ndege mzuri wanaoshambuliwa na kozi pande zote. Nenda ukawakusanye wanyama wote wakali waje kushiriki katika karamu. Neno: Bibilia Takatifu Je, urithi wangu haukuwa kama ndege wa mawindo wa madoadoa ambaye ndege wengine wawindao humzunguka na kumshambulia? Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni; walete ili wale. Neno: Maandiko Matakatifu Je, urithi wangu haukuwa kama ndege wa mawindo wa madoadoa ambaye ndege wengine wawindao humzunguka na kumshambulia? Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni; walete ili wale. BIBLIA KISWAHILI Je! Urithi wangu umekuwa kwangu kama ndege mwenye madoadoa? Ndege wakali wamemzunguka pande zote? Nendeni, wakusanyeni pamoja wanyama wote wa mwituni, waleteni ili wale. |
Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.
Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.
Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema BWANA; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.
Wanasimba wamenguruma juu yake, wametoa sana sauti zao; Nao wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; miji yake imeteketea, haina watu.
mimi nitawatia katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao, na mizoga yao itakuwa ni chakula cha ndege wa mbinguni, na cha wanyama wakali wa nchi.
Na mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi; wala hapana mtu atakayewafukuza.
Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; BWANA ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.
Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyamamwitu, wakatawanyika.
Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.