Wala msitoke nje mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba, hadi siku za kuwekwa wakfu kwenu zitakapotimia; kwa kuwa atawaweka muda wa siku saba.
Walawi 8:34 - Swahili Revised Union Version Vile vile kama ilivyotendeka siku ya leo, ndivyo BWANA alivyoagiza, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu ameamuru tufanye kama tulivyofanya leo ili tuwafanyieni ibada ya upatanisho. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu ameamuru tufanye kama tulivyofanya leo ili tuwafanyieni ibada ya upatanisho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu ameamuru tufanye kama tulivyofanya leo ili tuwafanyieni ibada ya upatanisho. Neno: Bibilia Takatifu Lile lililofanyika leo liliagizwa na Mwenyezi Mungu ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Neno: Maandiko Matakatifu Lile lililofanyika leo liliagizwa na bwana ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. BIBLIA KISWAHILI Vile vile kama ilivyotendeka siku ya leo, ndivyo BWANA alivyoagiza, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. |
Wala msitoke nje mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba, hadi siku za kuwekwa wakfu kwenu zitakapotimia; kwa kuwa atawaweka muda wa siku saba.
Nanyi mtakaa mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba mchana na usiku, na kuulinda ulinzi wa BWANA ili kwamba msife; kwani ndivyo nilivyoagizwa.
asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo;
ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake.