Basi wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu, wakainyunyiza madhabahuni; wakawachinja kondoo dume, na kuinyunyiza damu madhabahuni; wakawachinja na wana-kondoo, na kuinyunyiza damu madhabahuni.
Walawi 8:19 - Swahili Revised Union Version Kisha akamchinja; na Musa akainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose akamchinja na damu ya kondoo huyo akairashia madhabahu pande zake zote. Biblia Habari Njema - BHND Mose akamchinja na damu ya kondoo huyo akairashia madhabahu pande zake zote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose akamchinja na damu ya kondoo huyo akairashia madhabahu pande zake zote. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Musa akamchinja yule kondoo dume na kunyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Musa akamchinja yule kondoo dume na kunyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. BIBLIA KISWAHILI Kisha akamchinja; na Musa akainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. |
Basi wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu, wakainyunyiza madhabahuni; wakawachinja kondoo dume, na kuinyunyiza damu madhabahuni; wakawachinja na wana-kondoo, na kuinyunyiza damu madhabahuni.
Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za BWANA; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.
Kisha akamsongeza yule kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo.
Kisha akamkata kondoo vipande vyake; na Musa akateketeza kichwa, na vile vipande, na mafuta.